Madiwani wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa wamewafukuza kazi
watumishi wanane wa halmashauri hiyo kutokana na madai mbalimbali ikiwamo
ya utoro kazini
Madiwani hao
walifikia uamuzi hayo leo Mei 29 wakati wa kikao cha baraza la madiwani
Kikao hicho
kilitoa tamko ambalo lilisomwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sumbawanga ,
Kalolo Ntilia
Akisoma tamko
hilo, Ntilia aliwataja watumishi waliofukuzwa kazi kwa utoro kuwa ni pamoja na
John Chiza , Mfamasia, Ignas Mdigange, tabibu na Aisha Hida
muhudumu wa afya
Muuguzi,
Charles Joseph amefukuzwa kazi kwa kosa
la kutotii maagizo ya mwajiri wake na mwingine aliyekumba na panga hilo
ni mhudumu wa afya, Omari Komba
Nicas Kalolo ,Kaimu Mtendaji wa Kata yeye ameadhibiwa
kwa kushushwa ngazi ya mshahara kutokana na utovu wa nidhamu, Gasper
Gembe , Ofisa Mtendaji wa Kijiji amepewa onyo kali na kuamriwa kurejesha
Sh 755,000/- alizozitumia bila idhini ya mwajiri wake
Katika hatua
nyingine; Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Nyangi Msemakweli amewaagiza
watendaji wa vijiji kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wazazi 150 ambao
watoto wao wameshindwa kujiunga na elimu ya sekondari tangu walipofaulu,
Januari mwaka huu
Madiwani wawatimua kazi watumishi wanane
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment