Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), Patrick Ole Sosopi, amesema Wabunge wa CHADEMA kutolewa Bungeni sio kwasababu ya mapungufu yao bali ni uimara na uwezo wao wa kujenga hoja.
Sosopi ameyaeleza
hayo leo kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachoruka kupitia Ukurasa wa
'Facebook' wa East Africa Television, wakati akijibu swali la mtazamaji juu ya
wabunge wa chama chake kutojenga hoja na kuchangia Bungeni kama zamani.
''Tanzania kwasasa
tunakumbana na tamaduni mpya ya kisiasa, kwahiyo kutoona wabunge wa CHADEMA
wakichangia sio kosa lao, nimpe pole tu mtazamaji kwasababu haoni 'Bunge Live'
mana halioneshwi ila wabunge wako imara'', amesema.
Mwenyekiti huyo
amewatolewa mfano Mbunge wa Kibamba John Mnyika na Ester Bulaya wa Bunda, kuwa
wameonesha uimara na uwezo wao ndio mana wameondolewa Bungeni hivi karibuni
kwasababu watawala wanataka kusikia mazuri tu.
Sosopi ameongeza
kuwa wanatamani kuona uhuru wa kufanya siasa ukiendelea kama ilivyokuwa zamani
na sio kusubiri hadi wakati wa uchaguzi mwaka 2020 ndio wafanye mikutano ya
kisiasa.
Wabunge CHADEMA watetewa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 16, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 16, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment