Nchini Kenya rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta ameidhinisha
mswada wa sheria za uhalifu wa mtandaoni wa 2018 kuwa sheria.
Sheria hiyo itatoa adhabu ya faini ya dola 50,000/=, kifungo cha
miaka miwili jela au adhabu zote mbili kwa atakayetoa habari feki au mtu yeyote
atakayebainika kuwa na makosa ya mtandaoni.
Kadharika kwa mtu atakaye toa taarifa ambazo zinaweza kuzua
taharuki au kuzua vurugu sheria hiyo inasema atafungwa jela zaidi ya miaka
kumi.
Hatua hiyo imepokelewa kwa hisia na maoni tofauti kwa watu mbalimbali
ambapo kiongozi wa zamani wa chama cha wanasheria Kenya Apollo Mboya
amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kifungu hicho kinaweza kuwapa watawala
‘uhuru’ wa kukandamiza vyombo vya habari.
Kwa upande mwingine shirika la kimataifa la kutetea uhuru wa
wanahabari Committee to Protect Journalists (CPJ) nalo limekuwa likipinga
uidhinishaji wa mswada huo.
Kenya yapata mwarobaini wa uhalifu wa mtandaoni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment