Wachungaji watatu wamenusurika kichapo cha mbwa koko kutoka kwa
wananchi mara baada ya kushindwa kumfufua marehemu ambaye ni mwanakijiji
mwenzao baada ya wachungaji hao kudai wanauwezo wa kumfufua marehemu huyo
aliyefariki siku za chache zilizopita na kuzikwa katika makaburi ya kijiji
hicho.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Christopher Angelo, amesema tukio
hilo lilitokea Mei 7, 2018 majira ya saa 4 asubuhi .
Ambapo amesema wananchi walishikwa na hasira kubwa baada ya
wachungaji hao kuwapotezea muda ambao walitumia kwa siku saba usiku na mchana
kusali na kuomba bila mafanikio yeyote.
”Wananchi, ndugu na jamaa walikasirika kutokana na kuona kuwa
wachungaji hao wanawatapeli na kwa sababu waliwasababishia kuingia gharama
kubwa ya kulisha watu waliokuwa wakishiriki maombi hayo,” alisema.
Kwa mujibu wa Angelo, baada ya kuona hafufuki, ndugu wakiongozwa
na mama mzazi wa marehemu waliamua kwenda kutoa taarifa ofisi ya kijiji, ili
kuepusha vurugu ambazo zilitaka kutokea.
Mwenyekiti huyo alisema viongozi wa Kijiji baada ya kufika
kwenye eneo hilo walikuta ndugu wa marehemu wakiwa wanafoka kwa hasira huku
wakiwa wanawatuhumu wachungaji hao kuwa ni matapeli.
“Sisi uongozi wa Kijiji tulikuta vurugu na wananchi walikuwa
wanataka kuwapiga wachungaji hao, tulichofanya kuepusha shari ni kuwaondoa
wachungaji hao eneo hilo na kwa kweli walitii agizo hilo na kuondoka zao,”
alisema Angelo.Chanzo- Nipashe
Mwenyekiti ameongezea kuwa wachungaji hao watatu walifika kwenye
ofisi ya Kijiji na kujitambulisha kuwa wao ni wachungaji wanatoka katika Kijiji
cha Nsimbo na watakuwapo kijijini hapo wakiwa wameitwa na ndugu wa marehemu,
Raymond Mirambo aliyefariki dunia siku moja na kuzikwa kijijini hapo.
Wachungaji wanusurika kipigo baada ya kushindwa kumfufua mfu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment