Mwanaharakati wa haki za wanawake,
Germaine Greer (79) kutoka nchini Australia amesema kwamba watu ambao
wanapatikana na hatia kwa kosa la kubaka hawapaswi kupelekwa gerezani bali
wanatakiwa kupewa adhabu ya kufanyakazi za kijamii.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail,
mwanaharakati huyo amesema hayo jana Mei 30, 2018 akiwa Nchini Wales na
kuongeza kuwa ubakaji halitakiwi kuwa kosa la jinai kwasababu wanaofanyiwa
ubakaji wengi hawapati majeraha ya kimwili.
Mwanaharakati huyo ameongeza kuwa
wanaopatikana na hatia kwa kosa la ubakaji wanapaswa kuchorwa alama ya R katika
mkono au shavuni na kisha kutumikia adhabu kwa kufanya shughuli za kijamii kwa
saa zisizopongua 200.
“Ningependekeza labda wangechorwa
tattoo ndogo ingekuwa kitu kizuri, labda herufi R katika mkono au katika
shavu,na kufanyakazia za kijamii kwa saa 200 ningependekea hivyo” amesema Germaine
Mwanamama huyo amedai kwamba
alibakwa akiwa na umri wa miaka 18 na kuongeza kuwa hakuripoti tukio hilo
Polisi kwasababu alihisi angepoteza muda wake mwingi na pia ilikuwa ni fedheha
kusema hadharani kwamba amefanyiwa kitendo hicho.
“Wabakaji wasifungwe jela”-Mwanaharakati
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment