Mbunge wa Moshi Vijijini
Antony Kalisti Komu ameamua kuweka nadhiri ya kuachana na siasa na kurudi
kijijini kulima kwa kudai kuwa endapo katika uchaguzi mkuu wa 2020 watashindwa
kumtoa rais Magufuli madarakani.
Nadhiri hiyo ya Komu imewekwa wazi
na Katibu wa Itikadi na Uenezi ACT, Ado Shaibu ambaye amesema kwamba Mh. Komu
ameyatoa hayo ya moyoni mbele yake na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe
wakati wakiwa njiani kuelekea Kakonko kuupumzisha mwili wa aliyekuwa Mbunge wa
Buyungu Kasuku Bilago.
"Miaka ya tisini tulikuwa
na kizingiti cha kukabiliana na Nyerere. Yes, Nyerere campaigned against us,
nchi nzima. Sasa hawana Nyerere. CCM imevurugwa maradufu na inaendelea
kuvurugwa. CCM ya sasa si ile ya tisini au miaka iliyopita. Ni CCM mbovu
iliyosheheni wageni na kuwaweka kando wabobezi na wakongwe" Komu.
Ameongeza "CCM
ina-survive kwa nguvu ya dola na si nguvu ya hoja. Tukijipanga vizuri, tukawa
well organised, tukawa focused kwenye kusimamia masuala yao na kuyaongoza vyema
maeneo tunayoyaongoza, mambo yatabadilika. Jambo la msingi hasa nyinyi vijana
ambao mnafuatwa na mnarubuniwa rubuniwa ni kusimama imara"
Mh. Komu amesisitiza "Kwa
kweli mimi Magufuli tukimshindwa safari hii (2020) nitaachana na mageuzi na
kurudi kwetu kijijini kulima".
Mbali na hayo Mbunge huyo amewataka
wabunge wa upinzani kujipanga na kujua kutumia fursa ndani ya utawala wa rais
magufuli ili watanzania pasipo kujali vyama vyao waweze kuwaunga mkono.
Mbunge auweka 'rehani' Urais wa JPM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment