Mahakama Kuu ya nchini Kenya imezuia
matumizi ya vifungu kadhaa vya Sheria ya mtandao iliyopitishwa na kusainiwa
na Rais Kenyatta wiki mbili zilizopita nchini humo.
Mahakama imevizuia vifungu 26 vya
Sheria hiyo mpaka hapo shauri litakaposikilizwa, hatua hii inafikiwa baada vya
chama cha Wanahabari na waendeshaji wa Blogu kufungua pingamizi.
Akitoa uamuzi huo Jaji wa
Mahakama Kuu, Chacha Mwita amesema kuwa sheria hiyo ni kandamizi kwa haki
za binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 18
mwaka huu ambapo itasikilizwa tena.
Mahakama yapingana na Rais
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment