Mbunge wa Newala Vijijini Ajali
Akibar amemtaka waziri wa madini Anjela Kairuki kwenda Afrika ya Kusini
kutafuta wagnga wa kienyeji na kuwaleta nchini, ili kuweza kupata madini kwa
wingi,
Mbunge Akibar ameyasema hayo leo
alipokuwa akichangia hotuba ya Wizara ya Madini Bungeni, na kusema kwamba
amesikia kwamba madini yanatokana na mashetani, hivyo ni vyema Waziri akaenda
kumleta mganga aje kuagua.
“Siku moja tuliwahi kusikia kwamba
mambo ya madini yanatokana na mashetani, sasa hao mashetani ndio wanaofanya
nchi hii isipate madini, kama kweli sisi hatupati madini, basi nikuombe
Mheshimiwa Anjela aende South Afrika ukamlete Sangoma aje atuchinjie ili na
sisi tuweze kupata madini Tanzania”, amesema Mbunge wa Newala Ajali Akbar.
Mbunge huyo aliendelea kwa kulaumu
shirika la Stamico kwa utendaji mbovu, unaosababisha Tanzania kukosa mapato
yake kwenye sekta ya madini.
Mbunge amtaka Waziri amlete mganga
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment