Katibu Mkuu mpya wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema msimamo
wake kuhusu mabadiliko ya Katiba utakuwa tofauti na ule aliokuwa nao awali
kabla ya kuingia rasmi kwenye siasa za CCM kwa kuwa sasa ataendana na maelekezo
ya chama hicho
Mei 31 baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa katibu mkuu,
Abdulrahman Kinana, Dk Bashiru aliyekuwa akitetea mabadiliko ya Katiba amesema
msimamo huo aliutoa kwa kuwa alikuwa huru.
"Leo nazungumza
kama katibu mkuu, yaani swali lako lina majibu humohumo, ukiwa mchambuzi
unachambua kwelikweli. Ukiwa msemaji wa chama unawasilisha yaliyoamuliwa kwenye
vikao,"amesema Dk Bashiru
"Msimamo wa Halmashauri Kuu ndio chombo kikuu
kilichoniliteua na inaweza kunifukuza. Kwenye uchambuzi kule nisingeweza
kufukuzwa. Hapa kama wewe unanitakia mema, siwezi kuchambua yale ambayo
hayajaamuliwa na vikao
Hata hivyo, Dk
Bashiru amesema anaamini katika vyama kufuata Katiba zao kwanza na kuheshimu
Katiba ya nchi
Awali, Katibu
Mkuu mstaafu, Kinana amesema anampongeza Bashiru na kumtakia kazi njema
Dk Bashiru abadili msimamo Katiba mpya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment