Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Taifa, Ndg. Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wa CCM
kiujumla kumpa ushirikiano Katibu Mkuu mpya ambaye ni Dkt. Bashiru Ally kama
walivyo kuwa wanampa yeye kipindi alipokuwa kwenye nafasi hiyo.
Kinana ametoa kauli hiyo leo Mei 31,
2018 nje ya Ofisi ya CCM iliyopo Lumumba Jijini Dar es Salaam mara baada ya
kumaliza makabidhiano ya ofisi na kiongozi huyo mpya ndani ya chama hicho.
"Nimekuja ofisini hapa na
mwenzangu Katibu Mkuu CCM kufanya mambo matatu. La kwanza likiwa ni kumpongeza
kwa kuteuliwa na Mwenyekiti na kuchaguliwa na Halmashauri Kuu Taifa la pili ni
kumkabidhi ofisi na nimeshamkabidhi pamoja na makabrasha yanayohusika kwenye
ofisi na la tatu nilikuwa na kazi ya kumtambulisha kwa watendaji ili aone kazi
jinsi zilivyokuwa zikifanyika katika chama chetu na kuwaomba watendaji wampe
ushirikiano kama walivyofanya kwangu", amesema Kinana.
Ndg. Kinana ameng'atuka kwenye
nafasi hiyo siku za hivi karibuni huku akidai kilichopelekea kuchukua maamuzi
hayo ni kutokana na umri wake kuwa mkubwa hivyo anahitaji kupumzika katika
nafasi hiyo na kuwa mwanachama wa kawaida.
Kinana atoa kauli yake ya mwisho kwa wanaccm
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment