Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ambaye amebakiza siku chache kung'atuka
kwenye nafasi hiyo Dkt. Helen Kijo-Bisimba amedai akitoka hapo ataenda
kujihusisha na masuala ya uimbaji kwaya kwenye kanisa ambalo huwa anafanya
ibada.
Dkt. Kijo-Bisimba ametoa wakati
alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha East Africa Drive kilichorushwa Mei
30, 2018 kutoka East Africa Radio zikiwa zimepita takribani siku tatu tokea
kituo hicho kutangaza hadharani kustaafu kwa Mkurugenzi huyo pamoja na mtu
ambaye atashika nafasi yake mara atakapoondoka rasmi mwanzo mwa mwezi Julai.
"Kusema ukweli mpaka sasa hivi
natamani tu kupumzika. Mimi ni muimbaji wa kwaya hivyo nataka nitumie muda
mwingi katika kufanya kazi zangu za kanisani, najua kabisa bado nitaendelea
kushauri kazi yangu niliyokuwa nafanya", amesema Dkt. Kijo.
Msikilize hapa chini Dkt.
Kijo-Bisimba akielezea mpango wake wa kazi mpya atakazokuwa anajihusisha
nazo........
Hii ndio kazi mpya ya Dkt. Kijo-Bisimba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment