Zikiwa zimepita siku chache tangu ilipotokea kizazaa cha ng'ombe waliokufa kutaka kuingizwa sokoni, serikali imewaondoa hofu watanzania kuwa nyama inayopatikana nchini ni bora na yenye usalama wa kutosha na kwa namna yoyote hawawezi kula vibudu.
Kauli hiyo imetolewa
leo Mei 16, 2018 na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhanga Mpina Bungeni Jijini
Dodoma kwenye kikao cha 30 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, wakati akijibu la Mbunge wa Mbinga mjini Sixtus Mapunda aliyetaka
kusikia kauli ya serikali kuhusiana na jaribio la kuuza vibudu katika machinjio
ya Tegeta Jijini Dar es Salaam Mei 13, 2018.
Wakati anajibu swali
hilo Waziri Mpina amesema katika machinjio ya Tegeta walilikamata lori likiwa
na ng'ombe 54 kati ya hao 12 walikuwa ni mizoga ambapo mizoga hiyo minne
ilikuwa imeshachunwa na miwili ilikuwa tayari imeshakatwa katwa vipande.
"Vyombo vyetu
vya usimamizi, Mkurugenzi wa Mifugo, TFDA (Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini)
na Halmashauri tunao usimamizi madhubuti kwenye machinjio na mabucha yetu
katika kuzingatia usalama wa walaji hivyo basi watanzania wote wasipewe mashaka
wala hofu na mtu yoyote kwasababu nyama za Tanzania ni bora kwa namna yoyote
hawawezi kula vibudu", amesema Mpina.
Aidha, Waziri Mpina
amewashauri watanzania waendelee kula nyama za mifugo yao kwa kuwa vyombo vya
dola vipo na vinawahakikishia usalama wa kutosha katika masuala hayo.
"Kwa jaribio
hili tu tayari ameshafungiwa machinjio yake kutokana na jambo hilo kuwa
limefanywa kinyume na sheria za nchi hivyo Wizara yangu pamoja na Halmashauri
ya Kinondoni tulichukua maamuzi ya kuyafungia machinjio ya tegeta kwa muda
usiojulikana, kuiteketeza mizoga 12 na kuifukia pamoja kumkamata dereva wa lori
hilo pia bado tunamtafuta mmliki wa machinjio hayo kwa kuwa alikimbia baada ya
tukio kutokea", amesisitizia Mpina.
Kwa upande mwingine,
Mpina amesema mpaka sasa hivi serikali imewaondoa watumishi wote waliokuwa
katika kizuizi cha Kibaha na kupeleka wengine baada ya tukio hilo.
No comments:
Post a Comment