Benki Kuu ya Tanzania BoT, imeridhia uamuzi wa kuiunganisha Benki ya Twiga Bancorp Ltd na ile ya Tanzania Postal Bank Public limited Company (TPB Plc), ili iwe benki moja yenye nguvu ambayo utendaji wake utakuwa chini ya usimamizi na uendeshaji wa TPB Plc, uamuzi ambao utaanza Mei 17, 2018
Hayo
yamebainishwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu Dkt.
Bernard Kibese
wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo
Mei 16, 2018 na kusema benki hiyo ya Twiga Bancorp iliyokuwa chini ya usimamizi
wa benki kuu kwa takribani ya miaka miwili, ambapo mali za wateja na madeni ya
benki hiyo kwa sasa yatasimamiwa na benki ya Tanzania Postal Bank Public
Limited Company.
Dkt. Kabesema
amesema uamuzi huu umechukuliwa ili kuboresha uangalizi na utendaji wa benki
zinazomilikiwa na serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Benki Kuu ya
Tanzania inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye
amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.
Pamoja na hayo, Naibu
Gavana Kibese amesema hatua kama hiyo itachukuliwa pia kwa benki nyingine za
serikali ambazo ufanisi wake hautokuwa wa kuridhisha, kwani nia ya serikali ni
kuwa na benki moja kama sio chache zinazofanya vizuri, malengo ambayo Rais Dkt
John Pombe Magufuli amekuwa akisisitiza mara kwa mara.
Kwa upande wake
Meneja Uendeshaji wa Bodi ya Bima ya Amana, Bi Rosemery Tenga amewataka
walikuwa wateja katika benki ambazo zipo chini ya BOT kufuata mitaji ya benki
hiyo kuyumba kwenda katika benki hizo na utaratibu wa malipo utafanyika chini
ya usimamizi wa bodi ya Amana.
Uamuzi huo wa BoT
umetokana na benki ya Twiga kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji ambapo ni kinyume
na matwaka ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 na kanuni
zake ambapo kwa wakati huo ilihatarisha usalama wa sekta ya fedha.
No comments:
Post a Comment