Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya
Iringa, John Mpitanjia anayeendesha kesi inayomkabili mwanafunzi wa mwaka wa
tatu Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Abdul Nondo amegoma kujitoa katika kesi
hiyo kwa maelezo kuwa malalamiko ya mshtakiwa anayetaka ajitoe, hayana
ushahidi wa kutosha
Jana Mei 15, 2018 Nondo
aliiandikia barua Mahakama hiyo kumkataa hakimu huyo anayesikiliza shauri
lake, kwamba anamtilia shaka na ameona aiandike barua Mahakama ili itende
haki
Leo Mei 16, 2018 akitoa uamuzi huo
mdogo wa Mahakama, Mpitanjia amesema mahakama ni chombo cha mwisho cha
kutenda haki hivyo itaangalia usawa kwa pande zote mbili ikiwa ni
sambamba na kutoa haki kwa wakati bila kufungamana na upande wowote
Baada ya kutoa muamuzi huo hakimu
aliamuru upande wa jamuhuri kuendelea kutoa ushahidi wa mashahidi waliobaki
katika kesi hiyo
|
Hakimu agoma kujitoa kesi ya Nondo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment