Jeshi la Polisi katika
wilaya ya Gomba nchini Uganda linachunguza tukio la kuuawa kwa mwanamke
mjamzito aliyejulikana kwa jina la Amina Nabukeera (19) katika Kijiji cha
Bakandula.
Akisimulia tukio hilo mume wa
marehemu Bwana Arafat Kabuubi amesema tukio hilo limetokea jana Mei 15, 2018
muda wa saa mbili usiku wakati akiwa na mkewe wakielekea kununua mahitaji ya
nyumbani
“Mimi na mke wangu tulikuwa tunaenda
moja ya maeneo ya biashara muda wa saa mbili usiku kununua mahitaji ya
nyumbani, nilikua nikitembea mbele yake kabla sijasikia purukushani nyuma yangu
na nilipogeuka niliona mtu akimshumbulia mke wangu kwa kumpiga na nyundo
kichwani, alimkata sikio la upande wa kulia pamoja na taya kwa kutumia panga
kabla ya kukimbia. niliogopa sana na nilikosa nguvu za kumpigania mke wangu” amesema bwana Kabuubi
Bwana Kabuubi aliongeza kuwa
alijaribu kupiga kelele za kuomba msaada lakini alikua tayari amechelewa
kumuokoa mke wake ambae alifariki wakati akitafuta usafiri wa kumpeleka katika
kituo kidogo cha afya.
Mkuu wa Polisi katika mkoa wa
Katonga Kamanda Joseph Musana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuomba
wananchi kuwa watulivu wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa
kumbaini mtuhumiwa.
Hilo ni tukio la pili kwa marehemu
kushambuliwa ambapo mwezi Machi mwaka huu alishambuliwa akiwa nyumbani kwake
lakini alipatiwa matibabu katika kituo kidogo cha afya.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa
katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Gomba ukisubiri kufanyiwa uchunguzi wa
kidaktari.
Mume ashuhudia mkewe akiuawa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment