Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), imekamata malori mawili yenye bidhaa mbalimbali eneo la
Loliondo Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kupitia njia ya magendo yakitokea
nchini Kenya zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20.
Akizungumza leo jijini Arusha,
Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere amesema kuwa, malori hayo yenye namba
T 985 AJP na T 840 ABF yalikamatwa usiku wa tarehe 10 Mei, 2018 na kusisitiza
kuwa wafanyabiashara wenye bidhaa hizo wamevunja sheria kwa kuwa hawakulipa
kodi stahiki kama inavyotakiwa.
Kichere amefafanua kuwa,
wafanyabiashara wenye bidhaa hizi zilizokamatwa, wamevunja kifungu cha sheria
namba 82 na 200 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015 na Sheria ya
Forodha ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2004.
"Kwa ujumla bidhaa hizi
zote zina thamani ya shilingi 20,037,330.15 ambayo kodi ya bidhaa hizi ni
shillingi 28,524,758.11 na adhabu au faini ya bidhaa hizi ni shilingi
10,768,665.08. Hivyo jumla ya mapato
yanayotakiwa kulipwa Serikalini ni shilingi 39,293,423.19," Kichere.
yanayotakiwa kulipwa Serikalini ni shilingi 39,293,423.19," Kichere.
Ameongeza kuwa "Hivyo kwa
Sheria hizo, wafanyabiashara hawa wanatakiwa kulipa kodi pamoja na faini ya
shilingi milioni 39 na magari yao kutaifishwa".
Amezitaja bidhaa zilizokamatwa kuwa
ni pamoja na mifuko 362 ya sukari yenye uzito wa kilo 50 kila mmoja, maboksi 40
ya mafuta ya kula yanayoitwa Karibu, maboksi matatu ya mafuta ya kula yanayoitwa
Daria, magaloni 100 ya mafuta ya kula yanayoitwa Nyata na maboksi matatu ya
viungo vya mboga
Kufuatia tukio hilo, Kamishna Mkuu
Kichere amewakumbusha wafanyabiashara wote kuzingatia taratibu za uingizaji
bidhaa nchini ili kuepuka hasara kwenye biashara zao na kuongeza kuwa, TRA
haitavumilia ukiukwaji wowote utakaofanywa na wafanyabiashara kwa kutozingatia
sheria na taratibu hizo.
Serikali yapoteza Mil 39
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment