Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inakusudia kufanya mnada wa
wazi mwezi ujao kwa mizigo iliyokaa bandarini kwa muda mrefu bila kukombolewa,
ikiwamo ya Paul Makonda
Hata hivyo, ofisa wa TRA aliyetafutwa jana, hakutaka kueleza
kama jina la Makonda lililopo katika tangazo hilo ni la mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, na kiongozi huyo wa mkoa alipotafutwa, hakupatikana kuzungumzia suala
hilo
Haikuweza kufahamika kama shehena hiyo imetolewa katika muda
wa siku tano tangu tangazo hilo litoke kutokana na TRA kutotaka kuzungumzia
suala hilo kwa kina na kutopatikana kwa wamiliki
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa Mei 12 na Kaimu Kamishna
wa Forodha na Ushuru wa TRA, Ben Asubisye na kuchapishwa katika gazeti la
Serikali, Daily News, wamiliki wanatakiwa kuitoa mizigo hiyo ndani ya siku 30
kuanzia siku ilipotangazwa
Katika tangazo hilo lenye orodha ya makontena zaidi ya 800,
jina la Paul Makonda limejitokeza mara 20 akiwa mpokeaji wa makontena 20
yaliyopo katika bandari kavu ya DICD yakiwa na bidhaa kadhaa, kama samani
Ingawa hakuna uthibitisho kuwa Makonda ndiye mwenye
makontena hayo, Februari 16 mkuu huyo wa mkoa alikaririwa katika mtandao wa
gazeti la Serikali la HabariLeo kuwa alipokea makontena 20 yenye samani
zitakazotumika katika ofisi za walimu zinazoendelea kujengwa. Mzigo huo ulikuwa
sehemu ya shehena ya makontena 36
Samani hizo za ofisini zilizokuwa na thamani ya Sh2 bilioni,
zilitolewa na Watanzania wanaoishi Marekani wanaojulikana kama Six Region
Diaspora Council
Juhudi za kumpata Makonda ili kuzungumzia suala hilo
zilishindikana na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) hakujibu
Alipotafutwa na Mwananchi, mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa
Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema mamlaka imetoa notisi ya siku 30 kwa
waagizaji wa mizigo ambao mizigo yao imekaa bandarini kwa zaidi ya siku 90
“Tangazo lililotolewa ni notice (taarifa) kwa wahusika ili
wakomboe mizigo yao ndani ya siku 30. Isipokombolewa itanadiwa. Mizigo hiyo
inaweza kuwa ni ile ambayo haijalipiwa kodi au hata ile iliyolipiwa lakini
haijaondolewa,” alisema
Alipoulizwa kama shehena hiyo ni mali binafsi ya Makonda au
ya ofisi yake, Kayombo alisema: “Majina yaliyoandikwa kwenye magazeti ndiyo
taarifa za consignees (wapokeaji) zilizo kwenye nyaraka. Madhumuni ya matumizi
siyo sehemu ya wajibu wetu
TRA yatishia kuuza mali za Makonda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment