Wabunge wawili wa Chadema leo Mei 17, 2018 wamejikuta njia
panda baada ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kumzuia Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa kujibu maswali yao kwa madai kuwa si ya kisera
Waliomuuliza Waziri Mkuu maswali bungeni leo katika kipindi
cha maswali ya papo kwa hapo kiongozi huyo wa shughuli za Serikali
bungeni ni mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka Pauline Gekul (Babati Mjini
Gekul alimuuliza Waziri Mkuu kuhusu sera ya Serikali
ya mwaka 1996 ya kushusha madaraka katika halmashauri na lengo likiwa ni kuzipa
halmashauri nguvu, kubuni vyanzo vya mapato na kutumia
“Stedi ya mabasi ya babati ilipokonywa kwa madai kuwa ni
agizo la Rais na Rais amesema hahusiki bali ni viongozi wa Manyara, nini kauli
ya serikali,” amehoji Gekul
Baada ya swali hilo, Dk Tulia amesema si la kisera na
linaweza kujibiwa na waziri hivyo kumtaka kukaa na kutafuta swali jingine
Hata pale Gekul alipopewa fursa ya kuuliza jingine bado
amesema ,”ni swali la kisera, “ jambo lililomfanya Dk Tulia kumtaka aketi
Kwa upande wake Mwakajoka amesema kumekuwa na migogoro
katika halmashauri mbalimbali nchini kati ya wakuu wa wilaya na madiwani,
kutolea mfano Gairo, Malinyi na Mbeya Mjini.
Amesema katika
Halmashauri ya Tunduma kuna mgogoro ambao umesababisha baraza la madiwani
kutokaa kikao tangu Agosti 2017, kwamba licha ya maelekezo kadhaa ya waziri ila
mkuu wa mkoa na wilaya wanagoma kufanyika kwa kikao hicho
Kama ilivyokuwa kwa Gekul, Dk Tulia pia alipangua swali hilo
na kubainisha kuwa linaweza kujibiwa na waziri mwenye dhamana
Mara baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika,
Gekul amesimama kuomba mwongozo akitumia kanuni ya 68(7) akizungumzia swali
lake lilizozuiwa akisema ni swali la kisera, “Lakini lina maslahi kwa
umma kwa watu wa Babati na Naibu Spika hili swali limekwisha kufikishwa kwa
Waziri Mkuu na nyaraka tulishampatia, hili jambo limekuwa likisingiziwa Rais.”
Waziri Mkuu ni msimamizi wa shughuli za Serikali na Rais
kajivua hahusiki na mimi nimeuliza, nashindwa kuelewa, wabunge wengine
wanauliza suala la jimboni na anajibiwa, nikuombe mwongozo wako, suala hili
litaendelea hadi lini na suala la dhuruma mwisho hukurudia. Kwa nini meza
isimwache waziri mkuu ajibu maswali yetu badala ya kumchagulia?”
Akijibu mwongozo huo,
Dk Tulia amesema utaratibu waliojiwekea, kwamba maswali atakayoulizwa Waziri
Mkuu yana utaratibu wake na ya mawaziri ya nafasi yake, “kama waziri mkuu
analijua au halijui hilo si lenye mamlaka yangu.”
“Maswali ya majimbo yanaulizwa kwa mawaziri, maswali ya
kisera ambayo mawaziri hawawezi kujibu ndio anaulizwa Waziri Mkuu. Kanuni zetu
zimesema wazi maswali ya kisera au ya kijamii, kijamii si barabara ya jimbo
lako.”
Amesisitiza, “ Si swali la Gekul pekee hata la Mwakajoka
limezuiwa, swali la Tunduma waziri mkuu analijuaje. Niwasihi maswali kwa Waziri
Mkuu tujielekeze katika maswali ya kisera.”
Dk Tulia amzuia Waziri Mkuu kujibu maswali ya wabunge wa Chadema
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment