Mbunge
wa Mbeya kupitia CHADEMA Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu, amesema
alishangazwa na kitendo cha kusikia imepigwa simu kutoka juu, na kueleza kwamba
ni lazima yeye na Masonga wavae sare za jela
Akizungumzia suala hilo Sugu amesema
kwamba kitendo hicho kilimshangaza kwani kulikuwa kuna watu wengine wengi
walikuwa hawana sare na wamefungwa mule muda mrefu lakini walikosa sare, hivyo
kitendo cha kulazimishwa yeye ambaye yuko kwa muda mfupi kilikuwa
kinamshangaza.
“ Nisiite kujisikia
vibaya niite kushangaa, ni siku ambayo maagizo kutoka juu, ilipigwa simu
kwamba lazima Sugu avae uniform na Masonga, unaweza ukaona kwamba zaidi ya
wafungwa 600 hawana uniform, Sugu yuko pale mmemfunga kwa miezi mitano,
anatakiwa kutumikia kama miezi mitatu, lakini unamlazimisha avae uniform,
lakini kuna wafungwa pale wamefungwa maisha mamia kwa mamia hawana uniform, kwa
nini usiangalie namna ya kuwapatia wale uniform unahangaika na mtu ambaye
anapita tu!?”, amesema Sugu.
Sugu ameendelea kwa kusema kwamba
kitendo cha yeye kulazimishwa kuvaa sare hakikumkwaza kwani aliona inamsaidia
kuhifadhi nguo zake.
“Zilitafutwa siku hiyo hiyo
uniform, wakaja wakatuletea uniform ambazo zimevaliwa tukagoma, tukakataa kwa
sababu hatuwezi kuvaa nguo ambazo hatujui zimevaliwa na nani, wakaenda
kuhangaika kila kona sijui walitoa Segerea, lakini walitumia nguvu kuhakikisha
wanatuvalisha uniform, wao walidhani wakimvalisha Sugu uniform ataathirika
kisaikolojia, lakini we umeshanifunga kuvaa nguo ni kitu gani, kwanza
utanisaidia kutunza nguo zangu", amesema Sugu.
Sugu aliachiwa huru mapema wiki
iliyopita kwa msamaha wa Rais baada ya kutumikia kwa muda mfupi kifungo
chake cha miezi mitano katika gereza la Ruanda mkoani Mbeya, akiwa na mwenzake
Emmanuel Masonga
Alicholazimishwa Sugu kufanya akiwa gerezani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment