Nchi ya Burundi leo inapiga kura ya maoni
kufanya marekebisho ya katiba ambayo yanaweza kumuweka Rais wa sasa Pierre
Nkurunziza madarakani mpaka mwaka 2034
Kwa mujibu wa BBC Kura hiyo itapigwa
ya ndiyo au hapana ili kuongeza muda wa Rais kukaa madarakani kutoka miaka
mitano mpaka saba katika awamu moja.
Katiba ya sasa imeweka ukomo kwa
Rais aliyepo madarakani kuhudumu kwa kipindi cha awamu mbili, kwa mujibu wa
mabadiriko yatakayofanywa yatampa uhuru Rais Nkurunziza kugombea tena katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 akiwa kama mgombea mpya na hivyo huenda akatawala
mpaka mwaka 2034.
Chama tawala CNDD-FDD kinachoongozwa
na Nkurunziza ndicho kinaendesha kampeni ya kuunga mkono upigwaji wa kura ya
ndiyo huku kiongozi wa upinzani Agaton Rwasa chini ya mwamvuli wa muunganiko wa
vyama vya upinzani ujulikanao kama Amizero y’Abarundi wakihamasisha kura ya
hapana.
Nkurunziza kutawala burundi mpaka 2034
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment