Serikali imelazimika kuingilia kati
utekelezaji wa mradi mkubwa wa Maji wilayani Gairo uliokwama kwa zaidi ya
miaka nane kutokana na kutoa maji yenye chumvi kupita kiasi na
kumyang’anya mkandarasi aliyepewa kazi hiyo baada ya kushindwa kununua Mtambo
wa kuchuja Chumvi.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr. Kebwe
Stephen amesema Mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi billion 4.1 na
utekelezaji wake ulianza tangu mwaka 2010 na ulitakiwa kukamilika February 2012
lakini umeshindwa kukamilika baada ya kutoa maji yenye chumvi kupita
kiasi ambayo hayafai kwa matumizi ya binadamu.
Aidha Mhandisi huyo Heka Bulugu
amesema miongoni mwa changamoto zilizopelekea kukwama kwa mradi huo ni
kukosekana kwa huduma ya umeme katika maeneo yaliyopitiwa na mradi huo kwani
Mtambo wa kuchuja chumvi unatumia nishati hiyo.
Pamoja na hayo Serikali imeahidi
kununua mtambo huo baada ya mkandarasi kushindwa.
Serikali yamnyang'anya mkandarasi mradi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 28, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment