Matapeli watumia mradi wa bomba la kusambaza mafuta ghafi kutapeli.


Taasisi mbili za serikali ambazo ni Wakala wa Huduma  za Ajira nchini na Wakala  wa  Usajili,Ufilisi na Udhamini  RITA zimetoa tahadhari kwa umma kufuatia kuwepo kwa kundi la watu ambao wanatapeli watu kwa kutumia jina la Rais  kwa kutumia mitandao ya kijamii kuwa zipo ajira zimetangazwa katika mradi wa mkubwa wa ujenzi wa bomba la  kusafirishia mafuta ghafi na kuwataka kutuma taarifa zao na kisha kuwataka watoe  hela jambo ambalo siyo sahihi

Jamila Mbarook ni Afisa mawasiliano wa Wakala wa ajira ambaye anasema hakuna ajira zozote kwa sasa ambazo zimetangazwa na Rais wala serikali katika mradi huo na hivyo wanaotumia mitandao ya kijamii kuzitangaza ni matapeli na wala watu wasiombe

Naye Bw Jafali Malema kutoka RITA amesema hawana mtu yeyote ama wakala yeyote waliyempa jukumu la kutangaza ajira na hivyo ajira zilizotangazwa ni uzushi na zenye nia ya kuharibu taswira nzuri ya serikali

Baadhi ya wananchi wamesema utapeli wa namna hiyo na hasa katika mradi mkubwa kama huo wa kusafirisha mafuta lazima mamlaka husika ziongeze umakini ili kutovuruga malengo yaliyokusudiwa.

Matapeli watumia mradi wa bomba la kusambaza mafuta ghafi kutapeli. Matapeli watumia mradi wa bomba la kusambaza mafuta ghafi kutapeli.  Reviewed by KUSAGANEWS on May 28, 2018 Rating: 5

No comments: