Mahakama Kuu ya Mtwara imeondoa mahakamani shauri la
kupinga matumizi ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao (Online Content
Regulation) lililofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC) na wenzake dhidi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mbali na LHRC wengine waliopeleka zuio hilo ni Tanzania
Human Rights Defenders (THRD); Baraza la Habari Tanzania(MCT) na Jamii Media;
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa ); na Jukwaa la Wahariri
(TEF
Kanuni hizo zilipaswa zianze kutumika Mei 5 lakini mahakama
hiyo ikaweka zuio la muda Mei 4, baada ya kuwasilishwa kwa shauri la kupinga
mahakamani hapo.
Kesi hiyo namba
12/2018 ilisomwa leo Mei 28 mbele ya Jaji Mfawidhi, Dk Fauz Twaib na ilipangwa
kutolewa uamuzi juu ya mapingamizi matatu yaliyowasilishwa na upande wa
Serikali.
Akitoa uamuzi huo leo, Jaji Dk Twaib amesema mahakama hiyo
imekubali pingamizi moja kati ya matatu yaliyowasilishwa; kwamba mashirika
yaliyopeleka kesi mahakamani hapo hayana maslahi ya kutosha kwa maana ya
kufungua shauri hilo na kwamba hawakuonyesha namna moja kwa moja
yatakavyoguswa na kanuni hizo
Hivyo, mahakama iliondoa shauri hilo lakini inatoa nafasi
kwa mashirika hayo kama yatahitaji kupeleka shauri lingine kama
watajidhihirisha wana nafasi ya kufanya hivyo
Mahakama yaondoa zuio matumizi ya kanuni za maudhui ya kimtandao
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 28, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment