Akina mama 10 wamefariki dunia kutokana na madhara ya ukeketaji wilayani Ngorongoro


Akina mama 10 wa jamii ya kifugaji wilayani ngorongoro mkoani Arusha wamefariki dunia katika robo ya mwaka kuanzia mwezi januari mpaka march kutokana na ukeketaji unafanyika kwa siri wilayani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari,wakunga,maafisa maendeleo ya jamii pamoja na viongozi wa dini katika semina iliyoandaliwa na shirika la UNESCO wilayani humo Mratibu wa huduma za mama na mtoto Anna Masego amesema kuwa ukeketaji bado umekuwa changamoto na kuendelea kupoteza maisha ya mama wakatyi mwingine mtoto.

Katika semina hiyo inayotoamafunzo kuhusu kupinga ukeketaji dhidi ya mwanamke Masego amesema vifo hivyo vinatokana na madhara ya kukeketwa kwa mwanamke akiwa mdpogo na anapokuwa  baada ya mama kujifungua hutoa damu nyingi ambayo inampelekea kupoteza maisha  

Naye Mwenyekiti wa malaigwanan wilaya ya Ngorongoro Bwana Joseph Tiripai amesema Jamii ya kimasai imeacha tabia ya kufanya ukeketaji hadharani hivyo kufanya kwa siri bila mtyu kujua lakini pale wanapopata madhara hujitokeza ili kupata msaada wa matibabu,

Mzee Joseph amesema kwa mujibu wa taarifa alizopata kutoka kwa wanapofanya vitendo hivyo wanafanya kwa kuficha ambapo zamani ilikuwa wanafanya mpaka sherehe.

Laigwanan Joseph Ameongeza kuwa baadhi ya vijana wa kiume wameshaelewa madhara ya ukeketaji kwasababu mwanzo vijana hao walikuwa hawaoi mwanamke aliyekektwa lakini kwasasa wanaoa kutoka makabila tofauti.

Amesema kuwa serikali inaendelea kuwashauri akina mama wajifungulie vituo vya afya na jamii isaidie katika kumaliza tatizo hilo licha ya kuwa seriikali haiwez kufika kila mahali




Akina mama 10 wamefariki dunia kutokana na madhara ya ukeketaji wilayani Ngorongoro Akina mama 10 wamefariki dunia kutokana na madhara ya ukeketaji wilayani Ngorongoro Reviewed by KUSAGANEWS on May 28, 2018 Rating: 5

No comments: