Serikali imesema itawalipa mawakala wote wa pembejeo za
kilimo baada ya vyombo vya uchunguzi kukamilisha uchunguzi wa watumishi
waliodanyanga kuhusu malipo na uhakiki wa madeni unaendelea
Akijibu baadhi ya hoja za wabunge waliozitoa wakati
wakijadili bajeti ya wizara ya kilimo ya mwaka 2018/19, leo jioni Mei 16, 2018,
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema malipo ni mara baada
ya uchunguzi kukamika
“Nani kaiibia Serikali, katika maombi haya vyombo vya
uchunguzi vipo kazini, sisi kama wabunge wasimamizi wa rasilimali, vyombo vya
uchunguzi ni muhimu na kama ni mtumishi nani aliongeza sifuri katika milioni 20
ikawa bilioni, fedha si tatizo na tutawalipa wote wanaoidai Serikali,” amesema
Dk Kijaji
Kuhusu kutengwa kwa bajeti kidogo, Dk Kijaji amesema
Serikali inatambua umuhimu wa sekta ya kilimo lakini utengaji wa bajeti
unategemea rasilimali zilizopo
“Rasilimali ziko chache kuliko mahitaji, sote tupo hapa,
mlisema bajeti ya afya iongezwe, maji iongezwe na ifahamike Serikali inatoa
kipaumbele kwa kilimo na sisi tunatambua kuwekeza katika kilimo,” amesema Dk
Kijaji
Amesema miongoni mwa jitihada hizo ni kuiwezesha Benki ya
Kilimo: “Tumewekeza Sh60 bilioni na mpaka sasa wana Sh66 bilioni, wameweza
kuongeza kiwango hiki katika utendaji wetu na tumechukua mkopo zaidi ya Sh250
bilioni na kuipa benki hii.”
Akigusia benki hiyo kuwa jijini Dar es Salaam, amesema mwezi
huu itafungua tawi jijini Dodoma, Juni jijini Mbeya na Julai jijini Mwanza na
dhamira yetu ni kuwafikia wananchi kule waliko
Kwa upande wake, Naibu waziri wa Ofisi ya Rais- Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Joseph Kakunda ametoa maagizo kwa maofisa
kilimo kutoka ofisini na kwenda kuelimisha wakulima na wale watakaoshindwa
watachukuliwa hatua.
“Lazima wakulima
wapate haki yao ya elimu kuhusu kilimo na utaratibu wa kusubiri posho ili aende
kufanya kazi yake tumeshapiga marufuku,” amesema Kakunda
Kakunda amesema, “maofisa ushirika lazima wahakikishe
wanafanya mapitio ya vyama vya ushirika ili kujua kama utendaji ni mzuri na
kama ni mbovu wavifute na kuvisajili upya.”
“Maofisa ugani wafanye kazi ya kuwatambua wakulima wote ili
Serikali ifanye maandalizi ya haraka ya kuandaa pembejeo, walio chini ya
Tamisemi wapate huko hizi taarifa na uzembe hautavumiliwa,” amesisitiza
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa
Aweso amesema Serikali imetenga zaidi ya Sh29 bilioni kwa ajili ya kilimo cha
umwagiliaji na, “sisi kama wizara tutalisimamia hili na tunaahidi kushirikiana
vizuri na wadau wa wizara ya kilimo.”
Serikali: Malipo ya mawakala ni baada ya uhakiki
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment