Rais Dkt. John Magufuli ameagiza
kampuni tatu za mafuta ya kula kulipa asilimia 25 ya kodi baada ya kubaini
matanki saba kati ya yaliyokaguliwa yana mafuta safi yanayofaa kwa ajili ya
matumizi.
Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo leo
mchana Mei 15, 2018 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar
es Salaam na kusema mbali na kulipa kodi kampuni hizo pia zitatozwa faini kwa
kudanganya kuwa na mafuta ghafi wakati zikitambua kuwa ni masafi yanayofaa
kutumika.
Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kupeleka Bungeni muswada kwa
ajili ya kubadili sheria ya kodi ili wanaoingiza mafuta nchini watozwe kodi
kubwa kulinda viwanda vya ndani.
Katika ukaguzi uliofanywa na taasisi
za serikali, zikiwemo Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Shirika la Viwango
Tanzania, TBS, kwa kuchukua sampuli katika matanki mbalimbali, ilibaini kuwapo
matanki yenye mafuta safi na ghafi pamoja na malighafi ya kutengenezea sabuni.
Rais Magufuli agiza kupigwa faini kampuni tatu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment