Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo
Kayanza Peter Pinda amezitaka taasisi za elimu na mafunzo kuhakikisha mageuzi
ya kiuchumi yanafanyika nchini kwa kutoa elimu.
Mhe. Pinda ametoa ushauri huo jijini
Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Taaluma kuhusu nchi ya China
kijilikanacho kama Centre for Chinese Studies yaani CCS, kituo ambacho ni
sehemu ya taasisi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mh. Pinda amesema mageuzi ya
kiuchumi hususani kupitia ukuaji wa sekta ya viwanda, yanahitaji kuwa na jamii
inayopenda kufanya kazi kwa bidii na iliyo tayari kubadilika kifikra.
Uzinduzi wa kituo hicho umefanywa na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Augustine
Mahiga, ambaye amesema Tanzania ina uhusiano mzuri na nchi ya China lakini
inasikitisha kuona kwamba bado kama nchi haijatumia ipasavyo fursa ambazo taifa
la China imezitoa kwa Tanzania.
Aidha kituo hicho kilichozinduliwa
kimeelezewa kuwa jukumu lake ni kukuza uhusiano kati ya China na Tanzania
pamoja na kutumia mafanikio iliyoyapata nchi ya China kwa ajili ya kuharakisha
mageuzi ya kiuchumi.
Pinda atoa muongozo kuhusu Tanzania ya Viwanda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment