Muuguzi Mkuu wa Zahanati ya Kijiji na Kata ya Nyakasungwa,
Wilayani Sengerema, Mwanza, Grace Mashauri (50) amekutwa amefariki dunia ndani
ya nyumba yake
Grace alikuwa ni mtumishi pekee aliyekuwa akihudumia
zahanati hiyo, ambayo pia haina daktari
Diwani wa kata hiyo, Feruz Kamizula amesema alipata taarifa
hizo leo Mei 28, kutoka kwa watu waliokwenda kupata huduma ya matibabu katika
zahanati hiyo baada ya kukosa huduma kwa siku mbili mfululizo
“Baada ya kupata taarifa hizo leo mchana (jana) nilikwenda
katika zahanati hiyo ili kubaini tatizo nilipofika nilikuta mlango wa nyumba
umefungwa kwa ndani, lakini baada ya kuzunguka nyuma ya nyumba yake dirishani
ilisikika harufu kali,” alisema Kamizula.
Amesema baada ya kubomoa mlango wa nyumba yake walimkuta
muuguzi huyo akiwa amefariki dunia
Mkazi wa kijiji hicho, Esther Kazimili amesema walikwenda
Jumamosi Mei 26 katika zahanati hiyo kupata huduma lakini hawakufanikiwa
na waliporudi jana hali ilikuwa hivyo hivyo ndipo walipoamua kutoa taarifa kwa
diwani huyo
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Buchosa, Dk Ernest Chacha
amesema ofisi yake imepata taarifa ya kifo cha muuguzi huyo lakini chanzo cha
kifo chake hakijafahamika.
“Uchunguzi bado
unaendelea na mwili wake umepelekwa hospitali ya wilaya ya Sengerema
kuhifadhiwa,” amesema
Naye Mganga Mkuu wa Hospitari teule ya wilaya ya Sengerema
Sista Merry Jose amethibitisha kupokea mwili wa marehemu huyo na kwamba
umehifadhiwa katika chumba cha maiti na uchunguzi.
Kamanda wa PolisI Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema
hajapata taarifa za kifo hicho huku akiahidi kufuatilia
Muuguzi mkuu akutwa amefariki nyumbani kwake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 28, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment