Lema amjibu Gambo kwa waraka


Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amemjibu mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo  aliyesema lazima CCM italichukua jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020

Akizungumza Lema amesema hajashangazwa na kauli hiyo ya Gambo kwani ushindi wa uchaguzi siku hizi unategemea wasimamizi,  siyo wapiga kura

"Hatuwezi kukimbia, hatuwezi kwenda mafichoni, hatuna silaha na hatuwezi kubeba silaha kupambana dhidi yenu, ila kuwa na uhakika yakuwa tunatambua kuwaTaifa linapita katika majaribu makubwa," amesema.

Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita katika mkutano wa viongozi wapya wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) mkoani Arusha, Gambo alisema Jimbo la Arusha lazima litarudi CCM.

Leo Mei 28, Lema amemjibu Gambo kupitia waraka wake na amesema hajashangazwa na kauli ya mkuu huyo wa mkoa
"Ninafikiri watu wasiofahamu wanaweza kufikiri kauli hii ni ya bahati mbaya, kauli hii itakusaidia kulinda kazi yako kwa muda mrefu na itakupa heshima kubwa kwa watu walio juu yako," amesema Lema

Katika waraka huo, Lema amesema  mawazo yake kwa sasa hayapo kwenye uchaguzi wa 2020 bali kwa nchi yake na vizazi vijavyo
"Wakati wewe na kundi lenu mnawaza uchaguzi mimi ninawaza nchi yangu na maisha ya wajukuu wetu yatakuwaje baada ya sisi kumaliza mbio za maisha yetu hapa duniani, hasa baada ya kuona nchi yetu ina viongozi wengi kama wewe. " amesema.
Lema amjibu Gambo kwa waraka Lema amjibu Gambo kwa waraka Reviewed by KUSAGANEWS on May 28, 2018 Rating: 5

No comments: