Kinana aruhusiwa kung’atuka ukatibu mkuu CCM

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imepokea ombi la Abdulrahaman Kinana la kustaafu majukumu na nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM

CCM imepokea maombi hayo leo Mei 28 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM iliyoketi leo Jumatatu, Mei 28 Dar es Salaam

Katika kikao hicho NEC imeridhia ombi la Kinana na kwa pamoja wamemtakia mafanikio mema katika shughuli zake

“Napenda kumshkuru ndugu Kinana kwa utumishi wake katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na CCM itaendelea kutumia uzoefu wake katika majukumu mbalimbali ya chama kwa kadri itakavyohitajika,” amesema Rais John Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM.

Katika neno lake la kuwaaga wajumbe wa NEC Kinana amesisitiza wajumbe wa NEC na wana CCM kudumisha umoja

Kikao cha NEC kimeongozwa na Rais Magufuli na kilikuwa na kazi ya uchaguzi wa kujaza nafasi za wajumbe wa NEC kwa mujibu wa Katiba ya CCM Ibara 102

Wajumbe waliochaguliwa kuingia katika NEC kutoka Tanzania Zanzibar ni Afadhali Taibu Afadhali, Kombo Hassan Juma na Lailah Burhan Ngozi, kutoka Tanzania Bara ni Mizengo Pinda, Makongoro Nyerere na Khadija Taya (Keisha

Uteuzi na uchaguzi wa wajumbe hawa unakamilisha safu ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM yenye wajumbe 24 katika uongozi wa awamu ya tano mwaka 2017-2022.
Kikao hicho kinatarajiwa kuendelea tena kesho Mei 29


Kinana aruhusiwa kung’atuka ukatibu mkuu CCM Kinana aruhusiwa kung’atuka ukatibu mkuu CCM Reviewed by KUSAGANEWS on May 28, 2018 Rating: 5

No comments: