Watoto tisa wapelekwa Israel kutibiwa moyo

Watoto tisa wanaohitaji utaalamu zaidi wa tiba ya moyo wanaondoka leo Mei 28 kuelekea nchini Israel kwa matibabu

Akizungumzia safari ya watoto hao Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dk Naiz Majani amesema watoto ha wataambatana na wazazi na wauguzi.

 Amesema safari hiyo inahusisha watoto wenye umri wa miaka tisa hadi 14

Kadhalika amesema safari hiyo imeratibiwa na JKCI kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (SACH) ya Israel

"Taasisi yetu inatibu magonjwa ya moyo kwa asilimia 90 kwa watoto. Watoto hao hutibiwa na wataalamu wa ndani, hata hivyo tuna mkataba na Israel wa asilimia 10 ya wagonjwa wanaohitaji utaalamu zaidi kulingana na hali zao," amesema Dk Majani.

Amesema gharama za matibabu hayo zinagharamiwa na SACH.

Amefafanua kuwa watoto wanaoondoka leo kwenda kutibiwa nchini Israel ni kundi la sita tangu mwaka 2015 taasisi hizo mbili zilipoanzisha uhusiano huo

“Hadi sasa watoto 56 wameshatibiwa nchini humo,” amesema.

Mmoja wa watoto wanaoondoka leo kwenda kwenye matibabu Patrick Richard mwenye miaka 11 aliishukuru JKCI kwa msaada huo

"Nina matumizi mapya, shukrani kwa JKCI," amesema Richard

Watoto tisa wapelekwa Israel kutibiwa moyo Watoto tisa wapelekwa Israel kutibiwa moyo Reviewed by KUSAGANEWS on May 28, 2018 Rating: 5

No comments: