Mtanzania, Shujaa Suleiman Shujaa ameibuka kidedea katika
mashindano ya 19 ya kuhifadhi Quran Afrika na kujinyakulia kitita cha Sh15
milioni
Shujaa ameibuka mshindi katika kundi la washiriki wa juzuu
30 leo, Mei 27.
Pamoja na mamilioni
hayo, Shujaa mwenye miaka 23 ambaye ni mkazi wa Morogoro, amejishindia pia
laptop, kiwanja chenye hati eneo la Kigamboni kilichotolewa na kampuni ya
Property
International ya jijini Dar es Salaam pamoja na dola za Marekani 500
kutoka kwa Ahmed Seif “Magari” aliyetoa dola 500 kwa washindi wote watano
Akizungumza na maelfu ya waumini na Watanzania waliofurika
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo mchana Mei 27, 2018 Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kuilinda amani iliyopo nchini
kwani ikipotea hakuna atakayeweza kufanya ibada
“Mtakubaliana nami kuwa amani ya nchi yetu, ndiyo inatufanya
tutembee vifua mbele dhidi ya wenzetu, ni neema kubwa ambayo kila muumini
anapaswa kuilinda kwani ikipotea hata mkusanyiko wetu huu wa leo si rahisi
kufanyika mahali kama hapa,” amesema
“Leo hii tuko hapa uwanjani kwa sababu tuna amani, kama
Serikali isingekuwa inashirikisha Watanzania wote kulinda amani, basi
tusingeweza kukutanika hapa. Kuna nchi 18 ziko hapa, na watu wake wamekuja hapa
uwanjani kwa kuwa wana uhakika na amani tuliyonayo sisi Watanzania,” alisema
Mshindi wa pili kwenye kundi hilo la juzuu 30 ni Ahmed Noor
wa Sudan ambaye ameshinda Sh12 milioni pamoja na laptop akifuatiwa na Muzamil
Awadh Mohamed wa Sudan aliyejishindia Sh7.5 milioni pamoja na laptop
zilizotolewa na kampuni ya Camara Education
Mshindi wa nne ni Abdulally A. Mohammed wa Kenya aliyepata
zawadi ya sh. 5,711,000 na wa tano ni Ibrahim Maazur kutoka Niger, aliyepata
Sh3milioni
Washindi hao wote watano walipewa zawadi ya kwenda hijja na
Waziri wa Mambo ya Dini wa Saudi Arabia, Dk Saleh Ally Sheikh
Mtanzania Shujaa aibuka kidedea mashindano ya Quran Afrika
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment