Wabunge kumuaga Kasuku Bilago Jumanne


Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge kimesema kuwa, wabunge watauaga mwili wa mbunge wa Buyungu, (Chadema) Kasuku Bilago Jumanne, Mei 29, katika viwanja vya bunge.

Taarifa iliyotumwa leo, Mei 27 na Ofisi ya Bunge imesema kuwa kuagwa kwa Bilago Jumanne, kumeafikiwa baada ya bunge, Chadema na uongozi wa familia kukubaliana

“Baada ya waheshimiwa kutoa heshima zao za mwisho, mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Kakonko, Kigoma kwa mazishi,” imesema taarifa hiyo

Bilago amefariki jana, Mei 26 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa.
Wabunge kumuaga Kasuku Bilago Jumanne Wabunge kumuaga Kasuku Bilago Jumanne Reviewed by KUSAGANEWS on May 27, 2018 Rating: 5

No comments: