Mkuu wa Mkoa wa Magharibi Unguja,
Ayoub Muhammed Mahmoud ameziagiza Manispaa za mkoa huo kusitisha leseni ya
biashara za vileo katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao
waumini wa dini ya kiislamu duniani wameanza kufunga leo.
Akitoa tararifa kwa waandishi wa
habari Mh. Mahmoud amesema hatua hiyo imelenga kuimarisha imani za watu kwa
wanaofunga huku akizitaka manispaa ndani ya Mkoa huo kusimamia agizo hilo.
"Ili waumini waweze kuukabili
mwenzi huu kiukamilifu ni lazima kwa wananchi kutumia fursa za ramadhani kwa
kufanya mambo mema ili Mwenyezi Mungu aweze kuzikubali swaumu", amesema Mahmoud.
Aidha, Mahmoud amewataka watembezaji
watalii kutoa mwongozo kwa wageni kwa kufuata utaratibu ulio sahihi kwa kuvaa
mavazi ya heshima na yanayo kubalika kutokana na mila, silka na utamaduni.
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa
huyo ameliagiza Jeshi la Polisi kuongeza doria wakati wa jioni ili kuimarisha
hali ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao sambamba na kuimarisha usalama wa
barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima.
Mkuu wa Mkoa aagiza kusitishwa biashara ya pombe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment