Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF),
Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama
chake umekuwa ukiathiri utendaji wa viongozi (Wabunge) waliopatikana kwa chama
hicho kwa namna mbalimbali ikiwepo namna ya utendaji.
Akifanya mahojiano na www.eatv.tv,
Mtolea amesema kwamba mgogoro wa chama chake wakati mwingine unakuwa unawanyima
fursa wananchi kuweza kufahamu viongozi wao wanafanya kazi gani kwani mtandao
waliokuwa wanautumia kufikisha habari unakuwa umekatika.
"Mgogoro wa chama
unatuathiri kwa namna mbalimbali. Kwa mfano sisi wabunge mtandao wa chama
unakuwa umekatika. Wananchi wanakuwa wamekatika/wamegawanyika. Mbunge unakuwa
umefanya mambo mengi lakini wa kuyasemea kwa wanachi anakuwa hayupo kwa
kuwa ule mtandao tu ule mtandao tuliokuwa tunautumia unakuwa umekatika. Kwa
sasa mnasimama nyie wenyewe tofauti na ilivyokuwa awali" Mtolea.
Aidha, ameongeza kwamba "Kuwepo
kwa mgogoro kuwafanya mnakuwa hamfanyi kazi za chama zaidi ya kushughulikia
migogoro inayoendelea".
Mbali na hayo Kiongozi huyo amesema
mgawanyiko ndani ya chama umepelekea mzigo mkubwa wa ujenzi wa chama umehamia
kwa Wabunge ingawa pamoja na michango ambayo watakuwa wanaichangia bado
maendeleo ya chama hayataweza kwenda kwa kasi kama jinsi ambavyo wangekuwa
wanapata ruzuku.
Mgogoro wa Chama cha Wananchi CUF
unasadikika kuanza pale ambapo Mwenyekiti Prof. Ibrahim Lipumba alipotaka
kurejea kwenye nafasi yake ikiwa ni muda baada ya kujiuzulu kipindi cha
Uchaguzi mkuu 2015 kitendo ambacho kilisababisha wanachama kugawanyika huku
upande mmoja ukimuunga mkono Katibu wa Chama Maalim Seif Sharif Hamad na
wengine wakimuunga mkono Lipumba.
Mgogoro wa CUF unavyowaathiri wabunge wake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment