Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda, amebainisha kuwa baba yake ni moja kati askari kutoka Tanzania ambao
wamepigana vita nyingi kwaajili ya kutetea taifa ikiwemo vita ya kagera mwaka
1978.
Mh. Paul Makonda amesema hayo leo
Mei 17, 2018 wakati wa alipokuwa anatoa salamu kwa Rais Magufuli katika
sherehe za ufunguzi wa kituo cha uwekezaji cha SUMA JKT Mgulani Jijini Dar es
salaam na kuongeza kuwa alizaliwa na kulelewa katika kambi za jeshi
“Nikunong’oneze mheshimiwa Rais,
mimi nimezaliwa kambini na baba yangu ni miongoni mwa askari waliopigana vita
nyingi ikiwemo vita ya Uganda na mpaka ulemavu wake wa mguu ni kutokana na kazi
ya kuipigania Tanzania” amesema
Makonda
Makonda aliongeza kuwa kutokana na
kulelewa katika kambi za jeshi imemsaidia kupata ujasiri wa kuongoza mkoa wa
Dar es salaam wenye changamoto nyingi na kuweza kufanya kuwa Jiji la raha
Tanzania.
Katika tukio hilo, Rais Dkt Magufuli
alizindua kituo cha uwekezaji cha SUMA-JKT ambacho ndani yake kuna kiwanda cha
Ushonaji, Maji, Chuo cha Ufundi Stadi na Ukumbi wa Mikutano.
"Baba yangu alipigana vita ya Kagera" - Makonda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment