Gavana wa Mji Mkuu wa Kenya Nairobi
Mike Mbuvi Sonko amependekeza mwanasaisa wa upinzani anayekumbwa na utata
Miguna Miguna kuwa Naibu Gavana.
Sonko ametoa tangazo hilo ambalo
halikutarajiwa siku ya (jana) Jumatano jioni kwa njia ya barua kwa Spika wa
bunge la kaunti ya Nairobi, akisema Miguna Miguna ametimiza matakwa yote
yanayohitajika kikatiba.
Barua hiyo imekuwa ikisambaa kwenye
mitandao ya kijamii na kuzua maoni mengi kutoka kwa Wakenya, kutokana na kuwa
uteuzi wake umekuja wakati ambao haukutarajiwa kwa kuwa Bw Miguna amekuwa
mkosoaji mkuu wa Gavana huyo na kabla ya uchaguzi kwa kudai Sonko hana sifa
zozote za uongozi na hawezi kuongoza jiji la Nairobi.
Miguna alitarajiwa kurudi nchini
Kenya siku ya jana kutoka Canada baada ya kutimuliwa na serikali, lakini
akaahirisha safari yake akisema kuwa idara ya uhamiaji huikumpa pasipoti halali
jinsi ilivyoagizwa na mahakama.
Spika wa Bunge la Kaunti ya Nairobi
Beatrice Elachi amesema Bw. Miguna atahitajika kutatua masuala kuhusu uraia
wake na serikali ya Kenya kabla ya kuhojiwa na wabunge wa jimbo hilo.
Bw Miguna anahitaji kuidhinishwa na
bunge hilo kabla ya kuchukua wadhifa huo.
Hata hivyo Miguna mpaka sasa bado
hajazungumzia chochote kuhusu barua hiyo.
Miguna Miguna apewa shavu la uongozi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment