Shahidi atoa
mpya mahakamani, aeleza anayedaiwa kuuawa yuko hai mtaani Majumuisho ya Jamhuri
Hata hivyo,
akiwasilisha majumuisho ya upande wa mashtaka, Chavulla alieleza kuwa wameweza
kuthibitisha shtaka pasipo kuacha shaka na kwamba washtakiwa wote walishiriki
mauaji hayo
“Ni maoni yetu
kwamba, kwa ushahidi uliotolewa mahakamani na mashahidi wetu ni kwamba si
wengine walihusika kumuua Erasto Msuya bali washtakiwa waliopo mbele yako,”
alidai Chavula
Chavulla
anayesaidiana na Omary Kibwana, Kassim Nassir na Ignas Mwinuka aliongeza kuwa:
“Washtakiwa wote walihusika kupanga mauaji ya Erasto Msuya na wote walifika
eneo la tukio”.
Alieleza kuwa
ingawa washtakiwa wote walijitetea siku ya tukio hawakuwapo eneo la tukio,
lakini walishindwa kueleza walikuwa wakifanya nini ambacho kiliwazuia kufika
katika eneo la tukio
“Maeneo
waliyoyataja kuwa walikuwapo siku hiyo ya tukio inaonyesha kuwa wanaweza kutoka
na kuja hadi eneo ambalo mauaji yalifanyikia kisha kurudi walikokuwa,”
alisisitiza Chavulla.
Pia, alidai
washtakiwa wameshindwa kuleta mashahidi ambao wangeeleza siku ya tukio huko
walikokuwa, washtakiwa walikuwa wanafanya nini ambacho kingewazuia kufika eneo
la tukio.
“Tulitegemea kwa mazingira ambayo washtakiwa
walieleza walikuwapo, wangewaleta mashahidi ambao wangeieleza mahakama kweli
washtakiwa walikuwapo maeneo waliyoeleza na siku ya tukio
“Lakini hakuna
aliyeleta shahidi isipokuwa mshtakiwa wa kwanza
ambaye alileta mashahidi wawili
ambao nao walishindwa kuieleza mahakama siku ya tukio alikuwa wapi na alikuwa
akifanya nini,” alidai.
Mawakili wachuana kila mmoja upande wake kesi mauaji ya Bilionea Msuya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment