Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema Lawama za Mwenyekiti wa CHADEMA hazina
maana kwakuwa kiongozi huyo hakuwepo nchini kipindi Mbunge wa Buyungu Kasuku
Bilago anaumwa mpaka kuzidiwa na bunge kumsafirisha kutoka Dodoma mpaka
Muhimbili kwa matibabu.
Akizungumza kwa njia ya simu kwenye
kipindi cha East Afrika Breakfast, kinachorushwa na East Afrika Radio, Spika
Ndugai amesema ni vema akatafutwa mke wake ili aelezee namna ambavyo Bunge
limejitahidi kumtunza Marehemu, Tangu akiwa Dodoma, ikiwemo kusimamia gharama
za matibabu yake pamoja nakumtunza mke wake.
“Mimi nafikiri mumtafute mke wake,
yeye ndio anaweza kuwaeleza ana shukrani kiasi gani kwa Bunge, ambao ndio
tumemtunza tangu anaugua kule Dodoma, ambao ndio tumelipa gharama zote za
matibabu, ambao ndio tumekodisha ndege kutoka Dodoma kumleta Dar es salaam
mpaka Muhimbili, ambao ndio tumemtunza Muhimbili muda wote, mpaka amefariki
mikononi mwetu tukiwa tunamtunza mgonjwa na mke wake, ukishafanya yote hayo
halafu mtu mwishoni anakuja , yaani hakuwepo alikuwa nje ya nchi, anasema
kwamba wewe hakuna ulichokifanya, sasa wewe ujibuje, siuseme tu Haleluya
Inatosha.” Alisema Spika Ndugai.
Haya yanakuja ikiwa ni siku moja
imepita Tangu mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe atoe tuhuma kwa Bunge nakudai
kuwa halijashiriki ipasavyo katika kumuhudumia Marehemu, Bwana Mbowe ameyasema
hayo katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es salaam wakati wakuuaga mwili wa
Marehemu Bilago kabla yakupelekwa Bungeni Mjini Dodoma.
Spika amjibu Mbowe, asema 'Haleluya inatosha'
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment