Waandishi wa habari wa vyombo vya habari kutoka mikoa 4 ambayo
inavitendo vya ukeketaji wakiwa katika semina iliyaondaliwa na UNESCO
wakimsikiliza afisa mradi wa Unesco Rose Mwalongo
|
Mratibu wa huduma za mama na mtoto Anna Masago akitoa
elimu katika semina iliyoshirikisha waandishi wa habari,malaigwanan,watumishi
wa ustawi wa jamii na mangariba iliyoandaliwa na Shiriika la UNESCO
|
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ngorongoro Raphael Siumbu akizungumza
na washirikia ambao wameshiriki katika semina ya kupinga vitendo vya ukeketaji
ambao hawapo katika picha
|
Na Alphonce Kusaga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ngorongoro Raphael Siumbu
amesema watu wanaoweza kuwafanya wananchi kuacha mila potofu ikiwemo ukeketaji ni
wanasiasa lakini hawafanyi hivyo kwa kuhofia kutopata kura.
Akizungumza na waandishi wa habari,malaigwanani,waganga
wa jadi na mangariba katika semina iliyoandaliwa na shirika la Unesco Siumbu
amesema kuwa wanasiasa wengi wanashindwa kuionya jamii ili kuachana na mila
potofu kwasababu ya kuhofia nafasi zao za uongozi.
Amesema mila potofu hasa ukatili wa kijinsia umekuwa
tatizo kwa jamii ya kifugaji ikiwemo wilaya hiyo ya ngorongoro ambayo tatizo
hilo pia limepelekea kutokuwa na maendeleo kuanzia ngazi ya kijiji mpaka
wilaya.
“Kwahiyo kama 2016 tulikuwa na asilimia 66 na 2017 tuna
asilimia 81 na mpaka sasa tuna asilimia 86 mpaka hivi tunavyozungumza ,kwahiyo tunapanda
hivyo mpaka tutafika mahali ambao woote watakuwa wamekeketwa hii ni hali mbaya
kwa hiyo moja ya viashiria moja wapo vya maendeleo ni ukeketaji na Tuko nyuma
sana na hii inatokana na mawazo potofu wala si kitu kingine na watu wengine wa
kutusadia haya ni wanasiasa wanaotokana na jamii yenyewe lakini swali la
kujiuliza wamefanya nini kututoa hapa kwa hiyo kila siku hatushughulikii ishu
za maendeleo bali ni migogoro tuu tunashughulikia watu hebu tushirikiane hapa”Amesema
Mkurugenzi Siumbu
Naye mwenyekiti wa malaigwanan wilaya ya Ngorongoro Mzee
Joseph Tiripai amesema kuwa suala la ukeketaji anbayo ni mila potofu kwa jamii
hiyo ambayo wanaipinga ili zisiendelee na mwenye nafasi kubwa ya kuondoa imani
hizo ni jamii yenyewe kuamua na kukubali pamoja na wadau wamaendeleo kuingilia
kati.
Mzee Tiripai ameeleza kuwa ametembelea vijiji vya Ukuyan,Sukenya
na soitisambu lakini katika maeneo hayo wameogopa kukeketa kwa kuwa maeshaona
ni jambo ambalo lina madhara makubwa katika ukuaji wa mwanamke.
Katika taarifa yake Mratibu wa huduma za mama na mtoto
Anna Masego amesema wanawake 10 wa jamii ya kifugaji wilayani ngorongoro mkoani
Arusha wamefariki dunia katika robo ya mwaka kuanzia mwezi januari mpaka march
kutokana na ukeketaji unafanyika kwa siri wilayani humo.
Mkurugenzi Ngorongoro akasirishwa na Ukeketaji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment