Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, kwenye mchezo
wa ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya mabingwa Simba SC dhidi ya Kagera Sugar,
Jumamosi hii ambapo atawakabidhi Simba taji lao.
Hilo limebainishwa mchana huu na
Rais wa shirikisho la soka nchini Wallace Karia, ambaye ameweka wazi kuwa wao
kama shirikisho wameona ni vyema kumwalika Rais Magufuli kwenye tukio hilo
maalum na muhimu kwenye mchezo wa soka nchini.
''TFF kwa kupitia Ofisi ya Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, tumetuma ombi kwa Mh. Rais Magufuli kwaajili
ya kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo ili awakabidhi Simba taji la ubingwa na
tunaamini atakubali'', amesema.
Magufuli kuwakabidhi Kombe Simba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment