Wabunge Esther Bulaya pamoja Halima
Mdee ambao ni washtakiwa katika kesi ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 ikiwamo
kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kinyume cha sheria wameshindwa
kufika mahakamani leo kutokana na usafiri waliokuwa wakitumia kupata matatizo.
Hayo yamebainishwa na Wakili wa
utetezi, Peter Kibatala mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri,
kuwa sababu ya washtakiwa hao kutokuwapo mahakamani imetokana na usafiri
waliokuwa wanatumia kutoka bungeni mjini Dodoma kuelekea Dar es Salaam, kuwa na
tatizo na kusababisha wachelewe kufika.
Katika kesi hiyo ya jinai namba 112
ya mwaka 2018 inayowakabili viongozi tisa wa CHADEMA, akiwamo Mwenyekiti wa
chama hicho, Freeman Mbowe Halima Mdee , ni mshtakiwa wa saba, na Ester
Bulaya ni mshtakiwa wa tisa.
Mbali na Bulaya pamoja na Mdee
washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent
Mashinji , Mbunge wa Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa, Naibu makatibu wakuu Salum
Mwalimu (Zanzibar) na John Mnyika (Bara), Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko,
na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.
Viongozi hao wa CHADEMA wanakabiliwa
na mashtaka 12 katika hiyo ya kufanya mkusanyiko na maandamano yasiyo
halali Februari 16, 2018 yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline.
Bulaya na Mdee wakwama kisa usafiri
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment