Rais Dkt. John Magufuli amemuagiza
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kumpandisha cheo Kaimu Kamishna
wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA bandari ya Dar es Salaam Ben Usaje na
kuwa Kamishna kamili bandarini hapo ndani ya wiki hii.
Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo
wakati alipokuwa anazungumza viongozi mbalimbali kwenye bandari ya Dar es
Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya kushtukiza kwenye bandari na kusema
amefanya hivyo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya Ben Usaje katika kusimamia
maslahi ya nchi vizuri.
"Nawapongeza watu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) kwa kazi nzuri mnayoifanya, Waziri wa Fedha kampeni
tu huyu ukamishna kamili kwa sababu amesimamia haki halisi kwaajili ya maslahi
mapana ya nchi yetu, najua wanamchukia sana wengine wafanyabiashara lakini
waache wakuchukie Mungu anakupenda na watanzania tutaendelea kukupenda kwa hiyo
mka-confirm. Katibu Mkuu mkazungumze wote mumpe angalau ndani ya wiki hii
msimcheleweshe", amesema Dkt.
Magufuli.
Uamuzi huo wa Rais Magufuli umekuja
baada ya kumuuliza swali Kaimu Kamishna kuwa anafanya kazi gani TRA na ndipo
alipotoa amri hiyo ya kupandishwa cheo haraka kutokana na kuwa ameweza
kusimamia haki na maslahi kwa ufasaha.
Apandishwa cheo baada ya shitukizo la Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment