Rais Dkt John Magufuli amewataka
wananchi kuendelea kumuombea kwani kazi ya urais ni ngumu inahitaji maombi na
kuwataka waumini wa dini kiislamu kumuweka katika maombi hasa katika kipindi
cha kuelekea katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Rais Magufuli amesema hayo leo Mei
15, 2018 alipokuwa anaongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kufanya ziara ya
kushtukiza na kukagua shehena ya mafuta ya kula ambayo yalikua yamezuiliwa
bandarini hapo.
“Mama lishe na vijana mnaofanyakazi
nipo pamoja na ninyi, mimi ni yuleyule Magufuli sijabadirika, muendelee
kuniombea kazi hii ni ngumu sana ndugu zangu, inahitaji maombi hasa katika
kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ndugu zangu waislamu mniweka
kwa Mola muendelee kuniombea, Mungu awabariki sana nawashukuru sana”, amesema Rais Magufuli.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.
Magufuli ameagiza Waziri wa Fedha na Mipango na Waziri wa Viwanda kupeleka
muswada Bungeni kurekebisha sheria ya tozo ya mafuta yanayoingia nchini.
“Tulifanya makosa mengine upande wa
serikali bei ya mafuta ya kula na yale ya crude yote yanatozwa bei moja,
nimewaeleza Waziri wa Fedha na Wizara ya Viwanda wakafanye marekebisho Bungeni,
tunataka tujue kama ni crude, refined au double refined, tunataka tuimarishe
viwanda vyetu ili watanzania wengi wapate ajira” aliongeza Dkt Magufuli.
Katika ziara ya kusthukiza ya Rais
Magufuli bandarini hapo amebaini baadhi ya udanganyifu unaofanywa bandarini
hapo ikiwemo kukuta matenki manne yaliyokuwa na malighafi ya kutengenezea
sabuni tofauti na taarifa za awali ambazo zilisema kuna mafuta ya kula.
Kwa siku za karibuni kumekuwepo hali
ya sitofahamu baada ya meli mbili zenye shehena ya mafuta yaliyoagizwa na
wafanyabishara yenye jumla ya uzito tani 40,000 iliyozulilwa bandarini baada ya
ukinzani wa taarifa kati ya Shirika la viwango nchini (TBS) waliodai mafuta
hayo ni ghafi wakati upande wa mamlaka ya mapato (TRA) ikidai mafuta hayo ni
safi na yanastahili kutozwa kodi 25%
Kazi hii ni ngumu inahitaji maombi – Rais Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment