Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi
CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ameitaka serikali iliyopo madarakani visiwani
Zanzibar inayoongozwa na Dkt. Ali Mohamed Shein iwahurumie wananchi hasa katika
kipindi cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani.
Akizungumza na waandishi wa habari
katika Ofisi za CUF Vuga mjini Zanzibar, amesema kuwa waliopo madarakani wasiwe
hodari kuwataka wafanyabiashara wasipandishe bei za bidhaa wanazouza lakini na
wao kodi ambazo hazina tija, zinawakamuwa wananchi waweze kuzipunguza.
"Ni vyema kujifunza kwa serikali
ya Kenya ambayo imeweza kuondoa kodi kwa wafanyabiashara wale wote ambao
watafanya biashara ya tende katika Mwezi wa Ramadhani", amesema Maalim Seif.
Aidha, Maalim Seif amewataka
wananchi kufanya mambo ya kheri katika mwezi huo na kuacha kulumbana, kutoleana
maneno yasiyofaa kwani mwezi huo ni mwezi wa rehema hivyo ni vyema kufanya
mambo ya kheri yanayompendeza Mungu.
"Ni vyema kupendana,kusaidiana,
kuhurumiana,kuacha kugombana na kutohasimiana ili kupata fadhila za Mwezi
Mungu", amesisitiza Maalim Seif.
Kwa upande mwingine, Maalim Seif
amewataka wafanyabiashara wasiuchukulie kwamba mwezi wa Ramadhani kama ni msimu
wa kupata faida ya kupindukia na badala yake wauchukulie ni mwezi wa kuchuma
thawabu kwa lengo la kuwasaidia wananchi hasa masikini.
Maalim Seif aomba 'huruma' ya serikali
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment