Rais John Magufuli amemnyima fedha kijana mmoja aliyemuomba
kiongozi mkuu huyo wa nchi nauli, wakati alipokwenda kwa mamantilie eneo
la Bandari Dar es Salaam kunywa chai muda mfupi, baada ya kumaliza ziara yake
ya kushtukiza katika bandari hiyo
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Mei 15, 2018 wakati
akinunua mapapai na ndizi baada ya kukuta chai ikiwa imekwisha katika genge la
mamantilie huyo, huku kijana aliyekuwa akimsaidia mama huyo kupiga hesabu za
matunda hayo, kuchomekea suala la nauli
“Nataka mapapai nikale na wenzangu pale. Wewe mama jumlisha
bei ninunue tena wewe mhehe si ndio, unaona sasa mtani wangu wewe. Haya haya
hapa shilingi ngapi?,” amesema Magufuli akiuliza bei ya mapapai na kujibiwa
kuwa ni Sh22,000
“Na hizi ndizi ni kiasi gani, sawa kwa hiyo hizi ndizi zote
pamoja na mapapai ni Sh23,000 si ndio. Sasa mimi nakuongeza nakupa Sh30,000
kabisa, au hutaki hela yangu mama.”
Baada ya mama huyo kupokea kiasi hicho cha fedha, kijana
huyo alimuomba Rais nauli, “mheshimwia rais naomba nauli.”
“Hakuna nauli hapa nenda kalime,” amesema Rais Magufuli na
kuwafanya waliokuwepo eneo hilo kuangua kicheko
Ni kama kijana huyo alirudia tena kuomba nauli kwani rais
alisikika tena akisema, “hakuna cha nauli hapa.”
Magufuli amnyima kijana nauli, amtaka akalime
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment