Mchezo namba 226 wa Ligi kuu
Tanzania Bara kati ya mabingwa wa ligi Simba SC dhidi ya Kagera Sugar FC ya
Morogoro uliopangwa kuchezwa Mei 20, 2018 kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam umerudishwa nyuma na hatimaye kuchezwa Mei 19 mwaka huu majira ya saa 8
mchana.
Hayo yamebainishwa na taarifa
zilizotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura na kusema
sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuongeza ufanisi katika hafla ya kukabidhi
Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.
Simba itarajiwa kushuka dimbani siku
ya Jumamosi huku ikiwa na alama 68 baada ya mechi 68 huku Kagera Sugar ikiwa na
alama 31 baada ya mechi 28 ikiwa katika nafasi ya 10 kati ya timu 16
zilizoshiriki ligi kuu msimu wa 2017/18.
Kombe la Simba larudishwa nyuma
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment