Msanii wa BongoFleva mwenye 'hit
song' ya 'Mvumo wa Radi' Alikiba maarufu kama King Kiba amefunguka na kudai
yeye sio miongoni mwa wasanii wanaotegemea kupata pesa kutoka katika 'views' za
Youtube kama baadhi yao wanavyofikilia vichwani mwao.
King Kiba ametoa kauli hiyo ikiwa
zimepita siku kadhaa tokea video yake mpya ya 'Mvumo wa Radi' kushindwa
kuendelea kuhesabu idadi ya watu walioitazama jambo ambalo wengi wao walidai
kuna mchezo anafanyiwa msanii huyo ili asiweze kufikisha 'views' wengi
kama ilivyokuwa kawaida yake kila atowapo video.
"Hii ndio mara ya kwanza
kunitokea tatizo hilo ila halijaweza kuniathiri kwa namna yeyote ile. Ila
nashukuru watu wamepata walichokuwa wanastahili nasio kwamba mimi nategemea
pesa kutoka 'Youtube views', mimi nafanya muziki najua wapi napata pesa katika
muziki wangu. Nilichokuwa nahitaji kiukweli ni mashabiki zangu waridhike na
waelewe mimi ni msanii wa aina gani", amesema Alikiba.
Pamoja na hayo, Alikiba ameendelea
kwa kusema "tunajua kwamba kuna hizi biashara za kuweka ma-robot
katika 'Youtube' ili ionekane watu wana 'view' kwa wingi ila mimi binafsi
ninaona ni utoto tu. Haitokuja kutokea hata siku moja kwamba Alikiba ameweka
'robot' ili apate 'views' nyingi, mimi nafanya muziki wangu kwa ajili ya watu
na kwanini sasa nidanganye watu".
Wimbo wa Alikiba kwa sasa umetazamwa
jumla ya watu milioni 1.2 na kushikilia nafasi ya kwanza katika ya video
zilizotazamwa kwa kiasi kikubwa kutoka Youtube
Sitegemei pesa za 'views" - Alikiba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment