Rais John Magufuli ametoa
mwezi mmoja kwa taasisi za Serikali na watu binafsi wanaodaiwa Sh 41.4
billioni na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuhakikisha wanalipa fedha
hizo
Magufuli ametoa maagizo hayo leo alipokuwa
akizindua kituo cha uwekezaji cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), jijini
Dar es Salaam
Ametoa maagizo hayo baada ya Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi (CDF), Venance Mabeyo kumuomba kiongozi mkuu huyo wa nchi
kusaidia kulipwa kwa madeni hayo
Awali, Mabeyo alimueleza Rais
kuwa changamoto waliyonayo ni kutolipwa madeni na watu wanaofanya nao kazi
Amesema kupitia Suma JKT walitengeneza
na kukopesha watu mbalimbali na matrekta yenye thamani ya Sh40bilioni na
zilizolipwa ni Sh2 bilioni na kubaki deni la Sh 38bilioni
Ameeleza pia Suma JKT wanaolinda
taasisi za Serikali wanadai S 3.4 billion, hivyo kufanya madeni
hayo kwa Sh 41.4 billioni
"Tunaomba utusaidie kutia
msukumo katika hili kwa sababu taasisi za Serikali zina lugha ya tutalipa tu
endeleeni na ulinzi tu" amesema Mabeyo
Mabeyo amesema kuwa kutokana na hali
hiyo wanashindwa kuwalipa pamoja na gharama nyingine za kujikimu
"Waziri wa Ulinzi,
Katibu mkuu wa wizara ya Ulinzi waandikieni barua na mnitumie nakala ili niwe
nafuatilia watakapokuwa wameanza kulipa. Nataka fedha hizo zipatikane ili
ziweze kutumika kujenga viwanda vingine amesema Magufuli akijibu maombi ya
Mabeyo
"Mtu anaanzaje kuacha kulipa
fedha ya jeshi, hii ni dharau kubwa, raia wadharauliwe
na Jeshi pia?”
Katika hatua nyingine; Magufuli
ameagiza kuwa apelekewe majina ya maofisa waandamizi wa jeshi wastaafu ili
awateue kwenye bodi mbali mbali
JPM ATOA MWEZI MMOJA MADENI YALIPWE
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment