Jeshi la polisi mkoani Shinyanga
linawashikilia watu 12 kwa tuhuma za wizi wa maturubai ya magari makubwa ya
mizigo yanayofanya safari kupitia barabara ya Isaka Kahama kupitia Lusahunga
mkoani Kagera kwenda nchi jirani za Rwanda na Burundi huku mwingine mmoja
akishikiliwa kwa tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya aina ya mirungi
Akithibitisha kukamatwa watuhumiwa
hao na kushikiliwa na Jeshi la polisi kamanda wa Jeshi la polisi mkoani
Shinyanga ACP Simon Haule amesema watu hao wamekuwa wakifanya kazi hiyo
nyakati za usiku kwa kutumia pikipiki zisizo na taa na njia nyingine ya
kuwatumia wanawake wakijidai kama wanaomba lifti katika magari hayo
|
||
Baadhi ya madereva wa magari ya
mizigo ambao wamekumbwa na kadhia hiyo wametoa ushuhuda na kueleza namna wizi
huo unavyofanyika nyakati za usiku huku baadhi ya wamiliki wa makampuni ambao
wamefika katika kituo cha polisi cha Kahama na kutambua maturubai 34
yaloyofunguliwa na kuibwa katika magari yao
|
||
Kufuatia matukio hayo Kamanda
Simon Haule amewaonya wafanyabiashara na matajiri mkoani Shinyanga kuacha
tabia ya kununua mali zinazoibwa na kuuziwa kwa bei ndogo mitaani mwao
|
||
Watuhumiwa wanne waliokamatwa na
kushikiliwa kwa tuhuma za kufungua na kuiba maturubai katika magari ya mizigo
ni Daniel Juma, Philipo Osward,Emmanuel Bundala na Ngoya Samwel huku
mtuhumiwa wa dawa za kulevya aina ya mirungi akitwajwa kwa jina la Munashri Shock
Mohamed ambapo watuhumiwa 8 waliobaki majina yao yamehifadhiwa kwasababu za
kiintelijensia
|
||
12 mbaroni kwa wizi wa maturubai Shinyanga
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment